WANAFUNZI 140 WA SHULE YA SEKONDALI WANUSURIKA KUFA. - Rhevan Media

WANAFUNZI 140 WA SHULE YA SEKONDALI WANUSURIKA KUFA.

Wanafunzi 140,wa Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Petro iliyopo Manispaa ya Tabora,  wamenusurika kifo baada ya mabweni mawili kuteketea kwa moto wakati wakiwa madarasani,  ambapo hakuna kilichookolewa ndani kutokana na moto huo kushindikana kuzimwa, baada ya gali la zimamoto kuzama eneo la shule hiyo.
Mkuu wa Shule hiyo inayomilikiwa na Kanisa Agrikana Bw.Simon Peter Kyalla amesema kuwa, tukio hilo linawakumbusha machungu kwani mwaka jana 2015 mabweni mawili moja la wavulana, na la wasichana kwa nyakati tofauti yaliteketea kwa moto, na taarifa za tukio la sasa  hawajajua chanzo chake mpaka wafanye tathimini.
 
Kutuatia tukio hilo la mabweni kuwaka moto katika mazingira ya kutatanisha tena mchana kweupe, Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini Bw, Suleimani Kumchaya ameamua kuifunga shule hiyo kwa muda usiojulikana akidai kuwa, mpaka viongozi wa taasisisi hiyo wajihoji, si kilasiku ni tatizo la umeme.
 
Kwa upande wake,Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto mkoani Tabora  Bw.Kondo Mohamed ameasema kuwa, changamoto iliyowakumba ni mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Tabora pamoja na miundombinu duni ya barabara ambayo imesababisha gali lenye maji kuzama.  
 
Previous
Next Post »