WAKULIMA WA TUMBAKU KUTOA YA MOYONI. - Rhevan Media

WAKULIMA WA TUMBAKU KUTOA YA MOYONI.



Wakulima wa Tumbaku Mkoani Katavi, wamelalamikia kitendo cha mamlaka ya mapato nchini TRA kuanza kumlipisha kodi mkulima mmoja mmoja, badala ya utaratibu wa awali wa chama cha msingi kulipa kodi kwenye mamlaka hiyo, jambo ambalo linawaongezea mzigo wa gharama wakulima wanaowajibika pia kulipa ushuru wa mazao kwa Halmashauri husika.
Wakiongea na ITV mjini Mpanda wakulima hao wa zao la Tumbaku, wamesema hivi karibuni mamlaka ya TRA itaanza kuwatoza kodi wakulima wote ambao mapato yao ni zaidi ya shilingi milioni nne, jambo ambalo litawaongezea mzigo wakulima hao, na pia linaenda kinyume na azma ya Serikali ya awamu ya tano ambayo imekusudia kuboresha maisha ya wakulima, kwa kuwapunguzia mlolongo wa kodi mbalimbali.
 
Kwa upande wake Meneja wa mamlaka ya mapato kwa Mikoa ya Rukwa na Katavi Bw.John Palingo, amesema kodi hiyo ni kwa mujibu wa sheria, kwani kila mtu mwenye kipato anawajibika kulipa kodi bila ya kujali kundi analotoka.
Previous
Next Post »