WAGONJWA WAKOSA HUDUMA KWA SAA TISA SHINYANGA. - Rhevan Media

WAGONJWA WAKOSA HUDUMA KWA SAA TISA SHINYANGA.


Idadi kubwa ya wagonjwa waliofika kutibiwa katika kituo cha afya cha Tinde kilichoko wilayani Shinyanga wamekosa huduma kwa zaidi ya masaa tisa hali iliyomlazimu Mbunge viti maalum jimbo la Shinyanga vijijini Mh.Azza Hillaly akiambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw.Kiomoni Kibamba kufika katika kituo hicho na kutoa masaa 12 kwa mganga mkuu na wahudumu hao kutoa maelezo kwa maandishi kwanini hawakuhudumia wagonjwa hao hadi taarifa zikamfikia.
Akitoa agizo hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw.Kiomoni Kibamba amedai kuwa amechoshwa na malalamiko ya wananchi wanaodai kunyanyaswa na baadhi ya wahudumu huku akitoa onyo kali kwa mgamga mkuu wa kituo hicho Dr.Hellen kaunda kwa kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake na kutekeleza majukumu yake ya kikazi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa kituo hicho Dr.Hellen Kaunda amedai kuwa agizo la Mkurugenzi amelipokea lakini anasikitishwa na hali hiyo huku baadhi ya wauguzi wanaodaiwa kukaa katika wodi ya wanawake wajawazito bila kuwa na mgonjwa yeyote wakati wagonjwa wengine wakikosa huduma wamejitetea kwa kudai kuwa walikuwa hawajisikii vizuri.
Kwa upande wake Mbunge viti maalum wilaya ya Shinyanga Mh.Azza Hillaly amemtaka Mkurugenzi kumuondoa Mganga Mkuu wa kituo hicho Dr.Hellen Kaunda kwakua amekuwa akilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu lakini pia ameshindwa kusimamia utendaji kazi wa watumishi walioko chini yake.
Previous
Next Post »