WAGOMBEA URAIS WALIOSALIA KATIKA CHAMA CHA DEMOCRATIC WAJIBIZANA VIKALIKATIKA MDAHARO ULIOFANYIKA NEW YORK. - Rhevan Media

WAGOMBEA URAIS WALIOSALIA KATIKA CHAMA CHA DEMOCRATIC WAJIBIZANA VIKALIKATIKA MDAHARO ULIOFANYIKA NEW YORK.

Clinton SandersImage copyrightGetty
Image captionClinton amekuwa seneta New York naye Sanders ni mzaliwa wa jimbo hilo
Wagombea urais waliosalia katika chama cha Democratic, Hillary Clinton na Bernie Sanders, wamejibizana vikali katika mdahalo uliofanyika katika jiji la New York.
Kila mmoja ametilia shaka uwezo wa mpinzani wake kufanya uamuzi wa busara kuhusu masuala kama vile kudhibiti benki Wall Street, kudhibiti umiliki wa silaha na ujira wa chini.
Jimbo la New York litafanya mchujo wake Jumanne.
Bw Sanders amemkosoa Bi Clinton kwa kuunga mkono vita vya Iraq na kutetea mikataba ya biashara huru.
Lakini naye Bi Clinton amemtuhumu Bw Sanders na kusema hawezi kutekeleza hata sera zake mwenyewe, mfano kuvunja udhibiti wa benki kuu za Wall Street.
SandersImage copyrightAFP
Image captionSanders ameshinda majimbo saba kati ya manane yaliyofanya mchujo karibuni
Wote wawili wana uhusiano mkubwa na jimbo hilo la New York.
Bw Sanders alizaliwa huko naye Bi Clinton amekuwa seneta wa jimbo hilo kwa miaka minane.
Mdahalo huo wa runingani umefanyika eneo la Brooklyn.
Bw Sanders ameshinda majimbo saba kati ya manane yaliyofanya mchujo karibuni jambo lililomuwezesha kupunguza uongozi wa Bi Clinton katika mchujo wa chama hicho.
Clinton SandersImage copyrightEPA
Image captionClinton anajivunia uongozi mkubwa
Bi Clinton hata hivyo bado anajivunia uongozi mkubwa.
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika mwezi Novemba.
Previous
Next Post »