WACHINA TISA MBARONI KAGERA. - Rhevan Media

WACHINA TISA MBARONI KAGERA.



Kagera. Idara ya Uhamiaji imewanasa raia tisa wa China kwa kufanya kazi wilayani Kyerwa bila kuwa na vibali halali.
Kwa mujibu wa mkuu wa Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera, Abdalah Towo, raia hao waliajiriwa na kampuni ya George Joseph Kizenga Company Limited ya jijini Dar es salaam.
Waliokamatwa ni Changyuan Jia,Yongzhi Liu, Baoyin Qian, Bing Sunchen na Yuan Tangbao. Wengine ni Yuan Piangjing, Yuan Chi, Piangliang Yuan na Liu Huabao.
Akitoa taarifa ya utendaji kwa kipindi cha miezi mitatu (Januari hadi Machi), Towo alisema kuwa jumla ya raia 675 kutoka mataifa mbalimbali walikamatwa na wengine kufikishwa mahakamani.
Nchi za Rwanda na Burundi zinaongoza kwa kuwa na raia wengi wa kigeni waliokamatwa mkoani Kagera ambao huingia kupitia vituo vya Omurusagamba na  Kabanga kutokana na machafuko ya kisiasa. Katika kipindi hicho, jumla ya Wanyarwanda 137 na Warundi 353 wamekwishakamatwa.

Previous
Next Post »