VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAFURAHISHWA NA UAMUZI WA RAIS WA ZANZIBAR. - Rhevan Media

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAFURAHISHWA NA UAMUZI WA RAIS WA ZANZIBAR.


Klabu ya Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini imefurahishwa na uamuzi wa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kwa hatua yake ya kuwateua wawakilishi kutoka vyama vya upinzani, huku ikielezwa ni hatua za kuigwa na viongozi wote wa Afrika. Wakati Rais Shein akipongezwa kwa hatua hiyo ya kuunda Baraza la Mawaziri lenye mawaziri watatu wa vyama vya upinzani, baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameshauri CUF na CCM kuangalia uwezekano wa kumaliza mgogoro baina yao.Vyama tisa kupitia klabu ya viongozi vilivyompongeza Dk Shein ni ADA-TADEA, United Peoples Democratic Party (UPDP), Chausta na Sauti ya Umma (SAU). Vingine ni Chama cha Wakulima (AFP) na Chama cha Kijamii (CCK).Akizungumza kwenye hafla hiyo kwa niaba ya vyama vingine, Mwenyekiti wa Chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa alisema Rais Shein amejitahidi kufanya demokrasia ionekane kuchukua mkondo wake.Alisema hatua ya Dk Shein kuteua wawakilishi hao kuwa Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ni hatua ya kuigwa na kupongezwa kwani ameonesha ukomavu wa kidemokrasia.
Previous
Next Post »