UTAWALA WA MAGUFULI HAKUNA KUBEBANA HAPA KAZI TU. - Rhevan Media

UTAWALA WA MAGUFULI HAKUNA KUBEBANA HAPA KAZI TU.


Baada ya Rais Magufuli kumpiga chini mh Anna kilango Malechela aliyeteuliwa mwezi mmoja kuwa mkuu wa mkoa Shinyanga.Baadhi ya wamasiasa wa upinzani wameanza kumtetea.Kisiasa ni ishara mbaya kwa mama huyu kwani uchaguzi mkuu pia alipigwa chini ubunge jimbo la Same alikokuwa mbunge.



POLE SANA ANNE KILANGO MALECELA!
Mkuu wa Mkoa hata hajaanza Kazi, ameshafukuzwa. Kazi ya ukuu wa Mkoa si ya utendaji. Je kama watendaji walioko chini yake wamemdanganya?
Na kama Ikulu ilikuwa na Ripoti za kiintelijensia juu ya uwepo wa hao wafanyakazi hewa na imeona Mkuu wa Mkoa ni mgeni na hajawabaini, kwa nini Ikulu haimpi taarifa hizo Ili awashughulikie? Kwamba suluhisho ni kumfukuza tu.
Nitaandika zaidi kuhusu hatua za namna hii. Afrika inahitaji taasisi imara, siyo watu imara. Tatizo letu ni mfumo wa hovyo na siyo Mkuu wa mkoa mmoja mmoja. Kufukuza Kazi mtu mmoja mmoja siyo suluhisho la muda mrefu la uozo ulioko kwenye sekta ya Umma.
"HAPA KAZI TU"!
Mtatiro J.
Previous
Next Post »