TANZANIA KUPUNGUZA VIKWAZO VISIVYO VYA KIFORODHA. - Rhevan Media

TANZANIA KUPUNGUZA VIKWAZO VISIVYO VYA KIFORODHA.

Serikali ya Tanzania imeamua kupunguza vikwazo visivyo vya kiforodha ili kurahisisha huduma za biashara na usafirishaji kwa magari makubwa yanayosafiri kwenda nje ya nchi kwa kujenga vituo vya ukaguzi wa pamoja katika maeneo ya Vigwaza, Mikumi, Manyoni, Makambako, Nyakanazi na Mpemba.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga, amewaambia waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuwa mpango huo utapunguza usumbufu uliokuwa unatokea awali wa kusimama kila
kituo na badala yake kutakuwa na vituo maalum vya mizani vya kupima uzito.

Aidha, serikali imeandaa stika maalum zitakazobandikwa katika magari hayo kwa lengo la kutopata usumbufu watakapokuwa wanapita katika vituo vya mizani na mipakani kuelekea nchi za ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Soko la pamoja kwa nchi za Mashatriki na Kusini mwa Afrika (COMESA
Previous
Next Post »