TAMKO LA BUNGE KUHUSU UFISADI . - Rhevan Media

TAMKO LA BUNGE KUHUSU UFISADI .

Kumekuwa na taarifa zinazoendelea kupotosha umma na baadhi ya vyombo vya Habari kuwa Kamati ya Bunge yo Hesabu za Serikali (PAC) ilipokuwa ikitekeleza majukumu yake tarehe 5 April, 2016 ililitaka Jeshi Ia Polisi kuwasilisha Mkataba ulioingiwa Kati ya Jeshi hilo na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kuhusu mradi wa Utambuzi wa Alama za Vidole AFIS (Automated Fingerprint Identification System). Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili kwamba, taarifa hizo si za kweli na zina lengo Ia kupotosha umma kutokana na kile kilichoamuliwa na kamati hiyo.

Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba tarehe 5 April, 2016, kamati hiyo ilikutana na kujadili Taarifa ya Ukaguzi wa hesabu zilizokaguliwa za fungu 28, Jeshi Ia Polisi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2014 ambapo kamati pamoja na mambo mengine iliona kuna haja ya kupata maelezo ya kina kwa maandishi katika utekelezaji wa mkataba huo.

Kutokana na haja hiyo, kamati ilimwagiza Afisa Masuhuli ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ili kamati iweze kuchambua na kujadili maelezo hayo kabla ya kupendekeza kwa Bunge hatua zaidi za kuchukua. Kufuatia agizo hilo, kamati ilimwandikia pia Katibu wa Bunge taarifa kuhusu agizo hilo tarehe 12 Aprili, 2016 ili kupatiwa maelezo hayo kutoka kwa Afisa Masuhuli.

Ofisi ya Bunge ilimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo yo Ndani tarehe 12 Aprili 2016 kuwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kudumu yo Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotokana na kikao hicho cha tarehe 5 Aprifi 2016 kabla yo tarehe 18 Aprili, 2016 kama ilivyoshauriwa na kamati. 

Ni vyema Umma ukafahamu kuwa kilichoombwa na Kamati ni Maelezo ya utekelezaji wa Mkataba huo na sio Mkataba kama inovyoripotiwa na baadhi yo vyombo vya Habari ambapo Ofisi ya Bunge iliomba maelezo hayo yawasilishwe kabla yo tarehe 18 Aprili, 2016.

Imetolewa na:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge

DAR ES SALAAM

15 Aprili, 2016.
Previous
Next Post »