TAKUKURU WAINGILIA SAKATA LA MKATABA TATA WA KAMPUNI YA LUGUMI. - Rhevan Media

TAKUKURU WAINGILIA SAKATA LA MKATABA TATA WA KAMPUNI YA LUGUMI.



Mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises na jeshi la polisi limetua mikononi mwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) kwa ajili uchunguzi zaidi.


Msemaji wa takukuru, Tunu Mleli alisema kuwa, jalada ya uchungizi dhidi ya kampuni hiyo liko mikononi mwa takukuru ambapo wakimalisha watawasilisha kwenye mamlaka nyingine za kisheria kwa ajili ya hatua zaidi.

“Tayari tumeanza kazi ya uchunguzi wa kampuni ya Lugumi na jeshi la polisi… ikiwa tutamaliza, tutawasilisha mahakamani kwa hatua nyingine za sheria.

“Lakini kwa sasa siwezi kulizungumzia suala hilo kwa undani kwa sababu tayari limeanza kufanyiwa kazi,” alisema, Tunu.

Alisema, Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 37(1) hakiruhusu kuzungumzia masuala yanayochunguzwa mpaka yatakapokamilika.

Kampuni hiyo inadaiwa kuingia mkataba na jeshi la polisi mwaka 2011 ambako ilipewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchini kwa gharama ya Sh bilioni 37.

Lakini hadi sasa, kampuni hiyo imefunga mashine hizo katika vituo 14 tu katika jiji la Dar es Salaam huku kamuni tayari imekwisha kulipwa Sh bilioni 34 ambazo ni na asilimia 99 ya fedha zote.

Naye Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai(DCI), Diwani Athuman alisema ofisi yake imeiachia Takukuru kufanya uchunguzi kuhusiana na mkataba wa Lugumi kwa sababu ina mamlaka ya sheria kufanya hivyo.

“Suala la Lugumi tumewaachia Takukuru wafanye uchunguzi kwa sababu wana mamlaka ya sheria yakufanya hivyo na sisi tunaendelea kufanya uchunguzi wa mambo mengine yaliyojitokeza na yanayoendeleakujitokeza,”alisema Athuman.
Previous
Next Post »