TAFFA WAITAKA SERIKALI KUIANGALIA UPYA BANDARI. - Rhevan Media

TAFFA WAITAKA SERIKALI KUIANGALIA UPYA BANDARI.

Makamu wa Rais wa chama cha Forodha nchini Tanzania (TAFFA ) Bw Edward Urio amesema kuwa Serikali ya Tanzania ni lazima iangalie upya suala la mpango wa pamoja wa forodha baina ya Tanzania na Congo kwani mpango huo unaonekana kurudisha nyuma maendeleo ya bandari ya Tanzania.
Bw Urio ametoa kauli hiyo alipokuwa akiongea na East Africa Radio na kuongeza Kuwa kwa hivi sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa mizigo katika bandari ya Dar es salaam na wateja kuamua kutumia bandari nyingine za nchi jirani.
0

Akibainisha sababu nyingine zinazopelekea kupungua kwa wateja ni pamoja na ongezeko la VAT ya huduma wakati bandari nyingine hazina tozo hizo na kuwepo kwa taarifa kuwa kunaubadhilifu mkubwa unafanyika katika bandari za Tanzania.
Aidha kwa mwaka huu hawajapokea Meli za mbolea kwa wingi kama ilivyokuwa miaka mingine iliyopita na badala yake kutumiaBandari ya Mombasa, Beila na Darban.
Previous
Next Post »