SUMATRA WATOA TAHADHALI KWA USAFIRI WA NCHI KAVU NA MAJINI. - Rhevan Media

SUMATRA WATOA TAHADHALI KWA USAFIRI WA NCHI KAVU NA MAJINI.

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imetoa tahadhari kwa watumiaji wa vyombo vya majini na wasafirishaji kuacha kutumia vyombo hivyo katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na machafuko

ya hali ya hewa kwenye Bahari ya Hindi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hadi hapo hali itakapokuwa shwari.
Tahadhari hiyo iilitolewa na Ofisa Mfawidhi wa Sumatra, Dk. Walukani Luhamba, katika mahojiano na Nipashe mwishoni mwa wiki.
Dk. Luhamba alisema usalama wa maisha kwa wasafirishaji wa vyombo vya majini na abiria wao, utakuwa shakani
kutokana na machafuko ya hali ya hewa.
Pia aliwataka wavuvi kuwa makini na kufanya shughuli zao kwa tahadahari kubwa hasa kwa kuzingatia kuwa wengi wanafanya shughuli zao bila kuwa na vifaa vya uokoaji.
“Hali ya hewa imechafuka sana, ni hatari kwa wanaofanya shughuli zao baharini na ni vema wakasimamisha mpaka dhoruba itakapotulia kwa usalama wa maisha yao na abiria kwa wale wasafirishaji kwani vyombo vingi havina vifaa vya uokoaji,” alisema Dk. Luhamba.
Wakati huo huo, Sumatra mkoani Tanga inatarajia kuwafikisha mahakamani madereva wanne wanaofanya safari za Wilaya ya Lushoto kuelekea Tanga kwa tuhuma za kufanya safari za usiku kinyume cha taratibu, kanuni na
sheria za mamlaka hiyo.
Kwa mujibu wa Dk. Luhamba, madereva hao watafikishwa mahakamani leo ambapo sheria inawataka kulipa faini ya
kati ya Sh. 300,000 na 500,000 au kutumikia kifungo cha miaka miwili jela.
Alisema madereva hao walikamatwa katika operesheni maalum iliyofanywa na Sumatra na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani ambapo walikamatwa saa 10:00 usiku wakifanya safari kutoka mjini Tanga kwenda Lushoto.
“Wanajua kabisa muda wa kuanza safari ni saa 12 alfajiri, lakini kwa makusudi wameamua kukiuka sheria sasa tunawafikisha mahakamani wakajibu shtaka linalowakabili ili iwe mfano kwa wengine,” alifafanua Dk. Luhamba.
Previous
Next Post »