SHAMBULIZI LAUA WATU KADHAA AFGHANISTAN. - Rhevan Media

SHAMBULIZI LAUA WATU KADHAA AFGHANISTAN.

Image copyrightFB
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani anasema kuwa watu kadha wameuawa au kujeruhiwa kufuatia shambulizi la kujitoa mhanga wakati wa shughuli nyingi kwenye mji mkuu wa Afghanistan Kabul.
Walioshuhudia walisema kuwa watu kadha waliokuwa wamejihami, waliingia kwenye majengo yaliyo karibu na makao ya shirika la ujasusi la nchi hiyo.
Image copyrightAP
Image captionTaliban wamekiri kutekeleza shambulizi hilo
Baada ya kutokea kwa mlipuko, milio ya risasi ilisikika. Msemaji wa wizara ya ndani amesema kuwa eneo hilo limefungwa na vikosi vya usalama.
Taliban walitangaza kutekeleza shambulizi hilo. Wiki iliyopita Taliban walitangaza kuwa wangeanzisha mashambulizi kote nchini Afghanistan.
Previous
Next Post »