Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, inajitupa jioni ya leo kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, kuwakabili Mafalao wadogo wa Misri kwenye mchezo wa kirafiki wa marudiano.

Serengeti Boys walishinda mchezo wa kwanza kwa mabao 2-1 jumamosi iliyopita, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Bakari Shime amesema vijana wake wapo vizuri kuhakikisha wanaendeleza ushindi, ingawa wanajua mchezo unaweza kuwa mgumu kwa kuwa Misri watakuwa wamewasoma, na pengine kuja na mbinu mpya.
Serengeti Boys na Misri wote wanajiandaa na mechi za kufuzu michuano ya Afrika ya vijana itakayofanyika mwakani nchini Madagascar, ambapo Serengeti Boys itaanza kampeni za safari hiyo dhidi ya Shelisheli mwezi juni mwaka huu.
Sign up here with your email