
Rais John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta kutokana na kifo cha mke wa Rais mstaafu wa Kenya, Mama Lucy Kibaki aliyefariki dunia jana.
Mama Lucy Kibaki ambaye ni mke wa Rais mstaafu Mwai Kibaki alifariki dunia jijini London nchini Uingereza ambako alikuwa akipatiwa matibabu.Katika salamu hizo, Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na kifo hicho na kuongeza kuwa Kenya imempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yake.“Kupitia kwako Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta napenda kumpa pole nyingi Rais mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki, familia yake, ndugu, Jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu mkubwa,” alisema Rais Magufuli.Kwa muijibu wa taarifa ya Ikulu, Dk Magufuli pia amemuombea marehemu Lucy apumzishwe mahali pema peponi, Amina.Kwa mujibu wa Rais Kenyatta, Kenya imesikitishwa na kifo cha mama Lucy na inaungana na familia katika msiba huo mzito.
“Lucy amekuwa mgonjwa kwa kipindi cha mwezi mmoja. Alipatiwa matibabu hapa Kenya na baadaye kupelekwa Uingereza kwa ajili ya matibabu zaidi,” alisema Rais Kenyatta.Taarifa zinasema Lucy alilazwa katika hospitali jijini Nairobi tangu mwezi uliopita na kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Gertrude mjini Muthaiga.
Lucy ambaye ni mtoto wa Mchungaji wa Kanisa la Presbyterian la Afrika Mashariki, John Kagai na Rose Nyachomba, alizaliwa mwaka 1940 mjini Mukurwe.
Sign up here with your email
