NCHI ZA ULAYA ZAANZISHA MPANGO UKWEPAJI KODI. - Rhevan Media

NCHI ZA ULAYA ZAANZISHA MPANGO UKWEPAJI KODI.

Image captionNchi za Ulaya zaanzisha mpango ukwepaji kodi
Mashirika ya kifedha makubwa duniani yamekaribisha mpango wa nchi tano za Ulaya wa kupambana na ukwepaji kulipo kodi.
Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uhispania pamoaja na Italia sasa watabadilishana habari kuhusu umiliki wa kampnui za Shell na akaunti za siri.
Hatua hiyo ilipongezwa na mkuu wa shirika la fedha duniani IMF Christine Lagarde, ambaye alisema kuwa hatua hiyo ni kuongeza shinikizo kwa wale walio na nia ya kuficha mali.
Image copyrightAFP
Image captionKampuni ya Mossack Fonseca ililaumiwa kwa kusaidia ukwepaji kodi
Muungano wa kiuchumi na maendeleo OECD, ambao umetwikwa jukumu la kupambana na ukwepaji kodi, umesema kuwa nchi hizo ni lazmima zikabiliane na mawakili na mahakimu wanaoshiki katika kuficha siri.
Panama ambayo awali ilipinga shinikizo za kuitaka iwe na uwazi sasa imesema kuwa ina na ya kufanya mabadiliko.
Previous
Next Post »