NAIBU WAZIRI AZIFUNGIA HOSPITALI MBILI. - Rhevan Media

NAIBU WAZIRI AZIFUNGIA HOSPITALI MBILI.

[​IMG]
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamis Kigwangalla amezifungia hospital mbili tofauti zinazomilikiwa na Raia wa kigeni wakiwemo kutoka Korea kwa kile walichoeleza kuendesha huduma bila vibali maalum ikiwemo usajiri wa msajili wa hospital binafsi pamoja na ule wa msajili wa tiba mbadala. 

[​IMG]
Miongoni mwa vifaa vilivyokutwa ni pamoja na vile vinavyotumika mahospitalini na vingine vile ambavyo hawakuruhusiwa. 

Hospitali hizo zilizovamiwa na kukaguliwa ni pamoja na Korea Medical Clinic ya Kariakoo Mtaa wa Mahiwa na nyingine ni Oriental Traditional medicine clinic... Ambazo zote zinazomilikiwa na Mabong.

Dk. Kigwangalla ameeleza kuwa watu hao wamekuwa wakitoa huduma bila vibali halali huku pia wakiendesha huduma pasipo kufahamu lugha za kiswahili na Kiingereza.

[​IMG]



Previous
Next Post »