Hatimaye miili ya wachimbaji wadogo iliyo kuwa imefukiwa na maji katika mgodi wa dhahabu uliopo kijiji cha Mangae wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro imeopolewa yote baada ya jitihada za Jeshi la Zimamoto na uokoaji pamoja na wananchi zilizofanyika kwa zaidi ya saa 24 na kurejeshwa kijijini Mangae kwa ajili ya mazishi.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Betty Mkwasa amewataka wananchi wanaofanya shughuli za uchimbaji mdogo katika mgodi huo kusitisha mara moja huku wakisubiri utaratibu mpya utakaowekwa na serikali.
Naye Mwenyekiti wa kijiji hicho Berege Alex amelaani vikali hatua ya wawekezaji wanaochimba madini katika maeneo ya kijiji hicho kushindwa kutoa msaada wowote kijijini hapo pamoja na kuwa na idadi kubwa ya viwanja vya uchimbaji huku Mhandisi wa migodi Danieli Mdachi amesema nilazima watu wanaojishughulisha na uchimbaji wafuate taratibu na sheria zilizopo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja waliofariki kwa majina huku akiwataka wachimbaji wadogo kuwa na uangalifu kuingia migodini hasa kipindi hiki cha mvua zinazo endelea kunyesha.
Sign up here with your email