MGOMO wa kisiasa unaoendelea Kisiwani Pemba juzi ulichelewesha kwa muda wa saa kadhaa mazishi ya marehemu Bi Achia Khatib wa Mjini Wingwi Wilaya ya Micheweni , baada ya msikiti uliokuwa utumike kuswalia mwili wa marehemu kufungwa kwa kufuli .
Mbali na kitendo cha kufungwa kwa msikiti huo , pia baadhi ya vifaa vilivyokuwa vitumike katika mazishi hayo kufichwa ikiwemo kitanda (jeneza) pamoja na mitaimbo ya kuchimbia kaburi kwani sehemu hiyo ni ya mawe .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mmoja wa wanafamilia , Said Omar Said alisema kuwa hali hiyo ya sintofahamu ni imetokea ikimhusisha mtoto mkubwa wa marehemu Abdalla Kombo ambaye ni Mwenyekiti wa CCM kijijini hapo .
Alifahamisha kwamba wananchi waligoma na kusababisha kufungwa kwa msikiti , wakidai kwamba hawako tayari kushiriki mazishi , hadi pale mtoto wa marehemu (Mwenyekiti wa CCM) atakapoondoka katika msiba huo .
“Unajua mzee wetu alikuwa ni mfuasi wa CUF , lakini sasa mtoto wake mkubwa ni mwanaCCM , hivyo alitaka aondoke ili washiriki mazishi hayo ”alieleza Said Omar Said kwa maskitiko .
Sheha wa Shehia ya Mjini Wingwi Shehe Yussuf Hamad aliiambia gazeti hili kwamba , wananchi hao walitaka pia kuzuia makaburi yasitumike kumzika marehemu , lakini serikali ya kijiji ililazimika kutumia nguvu kutumika kwa makaburi hayo .
Alisema kwamba visa vingi vya maajabu vilitokea katika msiba huo , kwani hata sindano ya kushinea sanda ilichukuliwa na mtoto mdogo wa marehemu Hamad Kombo na kuifichwa wakati kazi ya ushinaji wa sanda ikiendelea.
Hali hiyo iliwafanya ndugu na jamaa wa karibu kuomba msaada kutoka vijiji jirani ikiwemo Micheweni na Majenzi , ambapo wakaazi wa vijiji hivyo ndio waliosaidia kupatikana sanda na kitanda cha kubebea mwili wa marehemu .
Imamu wa msikiti wa Ijumaa katika Shehia hiyo Bakar Abdalla alipotafutwa kwa njia ya simu alikana kuhusika na kitendo cha kufungwa msikiti , na kusema hata taarifa za kuvunjwa kufuli hajazipata .
Aidha alifahamisha taarifa za kifo cha bibi huyoa anazo , lakini taarifa za wapi swala ya kumswalia maiti itafanyika katika msikiti huo hakuwa na taarifa .
“Taarifa ya kifo nilizipata lakini sehemu ambayo swala itafanyika sikuwa na naelewa , mimi nafahamu kwamba ulikotokea msiba kuna msikiti mwengine mdogo na ndio uliotumika kumuswalia maiti ”alieleza.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mwenyekiti wake Abeid Juma Ali ilifika katika eneo la tukio na baada ya mazungumzo na baadhi ya wazee katika shehia hiyo yaliyochukua muda wa saa mbili , walilazimika kuvunja kufuli katika msikiti huo .
Akizungumza na baada ya tukio la kuvunja kufuli , Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo alilaani kitendo hicho na kuwataka wananchi kushirikiana na pamoja katika shughuli za kijamii .
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alikemea nyumba za ibada kutumika kwa masuala ya siasa na kuahidi kulitafutie ufumbuzi suala hilo kwa kukutana na mashekhe wote na maimamu wa misikiti yote Wilayani hapa .
“Hichi kitendo kwa kweli si cha kiungwana huwezi kumsusia maiti kwa misingi ya kisiasa , nimepanga kukutana na mashekhe wote wa wilaya tulizungumzie ikiwezekana kuweka maazimio lengo ni kudumisha upendo “ alieleza.
Mazishi hayo ambayo yalipangwa kufanyika majira ya saa saba za mchana , yalifanyika saa kumi na moja za jioni baada ya wanaccm kutoka shehia na vijiji jirani kufika na kusaidia shughuli za kuustiri mwili wa marehemu .
UHURU WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI
…………….
Wanadamu wameumbwa kwa hulka na silika ya kuwa na uwezo wa kuwasiliana miongoni mwao, jamii wanamoishi, taifa na hata ulimwenguni ili waweze kutimiza nia na azma yao ya kuwasiliana.
Ili mawasiliano hayo yakamilike ni lazima yabebe ujumbe unaokusudiwa kufikishwa katika jamii.
Ujumbe huo ili uweze kumfikia mlengwa, ni lazima iwepo njia ya kuufikisha ujumbe huo kwa mlengwa ambao huwasilishwa kwa maandishi (magazeti), sauti (redio) na picha (TV) pamoja na mitandao ya kijamii kupitia huduma ya inteneti.
Vyombo hivyo vya habari vinahusisha wataalamu ambao kazi yao ni kuhakikisha jamii inapata ujumbe kwa wakati ili kuweza kujenga, kuboresha na kuimarisha maisha yao kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni.
Vyombo vya habari hakika vimekuwa ndio macho na masikio ya wananchi ili kufikisha ujumbe unaohusu mambo mbalimbali yanayofanyika ndani na nje ya nchi.
Tunapoelekea siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Mei 2 na 3, maadhimisho hayo mwaka huu yataadhimishwa nchini Finland, ambapo wanahabari wote duniani wataungana kuwakumbuka wenzao waliofariki dunia walipokuwa wakitekeleza majukumu yao na kupanga mipango mipya ya namna watakavyoboresha kazi zao ziwe za ufanisi zaidi.
Tanzania ikiwa miongoni mwa mataifa ya dunia hii, nayo haipo nyuma katika suala la uwepo wa vyombo vya habari.
Ni dhahiri vyombo vya habari nchini vimekuwa kiungo muhimu katika kisaidia Serikali kutoa taarifa mbalimbali na ajira hatua ambayo imesaidia kupunguza tatizo la ajira nchini.
Ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki, Tanzania inayoongoza kwa kuwa na vyombo vingi vya habari, hali ambayo ni msingi wa kuajiri watu wengi zaidi katika tasnia hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ambaye ndiye mwenye dhamana ya habari nchini anasema Serikali inaunga mkono juhudi zinazofanywa na vyombo vya habari nchini.
“Tulipofika ni pazuri ukilinganisha na tulipotoka, mengi yamefanyika hasa ukiangalia idadi ya vyombo vya habari nchini na uhuru wa waandishi wa habari wanavyoanadika na wanavyofikisha ujumbe kwa wasomaji, wasikilizaji na watazamaji” alisema Waziri Nape.
Aidha, Waziri Nape amesema kuwa bado Serikali inakusudia kuboresha mazingira ya waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa hali ya uhuru hasa wanapotimiza majukumu yao ya kiundishi wa habari.
Kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambacho ni chombo kilichoanzishwa kisheria kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji nchini hadi sasa kuna jumla ya vituo kadhaa vya radio na televisheni vilivyosajiliwa.
RC RUGIMBANA AONGOZA KONGAMANO LA MIAKA 52 YA MUUNGANO UDOM
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Lugimbana akizungumza na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM -UDOMASA), wakati wa mdahalo wa miaka 52 ya Muungano uliofanyika katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo UDOM leo. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Professa Idrissa Kikula.
Mwenyekiti wa Jmuiya ya Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA), Mhadhiri Msaidizi, Edson Baradyana akitoa shukurani kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Lukimbana kwa kukubali kufungua kongamano hilo.
Baadhi ya wanachuo na wanataaluma wakishiriki kwenye kongamano hilo la miaka 52 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Jopo la wawezeshaji wa kongamano hilo
Sign up here with your email
