Timu ya Mgambo Shooting imesema unauhakika wa kuendelea kubaki katika michuano ya Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara kwa msimu ujao kwani nafasi waliyopo kwa sasa sio mbaya.
Kikosi cha Mgambo JKT cha jijini Tanga
Katibu Mkuu wa Mgambo Shooting Steven Kaaya amesema, wamebakiwa na mechi mbili za nyumbani ambazo ni dhidi ya JKT Ruvu na Mtibwa Sugar ambazo wanaamini wanashinda na kuendelea kubaki katika Ligi.
Kaaya amesema, hawajafanya vibaya sana kwani nafasi waliyopo ndiyo nafasi yao kwa misimu yote na kukaa katika nafasi za juu katika ligi sio nafasi zao.
Mgambo Shooting ambayo ilipoteza kwa Yanga hapo jana Uwanja wa Taifa jijini dar es salaam baada ya kuchapwa bao 2-1 inashikilia nafasi ya tatu kutoka mwisho.
Sign up here with your email
