ANGOLA Imekumbwa na Shambulio la kimtandao kutoka katika kundi la wahalifu mtandao wajulikanao kama “Anonymous” ambapo tovuti 20 za serikali ya Nchi hiyo zimefanikiwa kuangushwa na kundi hilo la kihalifu mtandao.
Tukio hilo lilitokea kufuatia shinikizo la kuachiwa huru watu 17walioshikiliwa nan chi hiyo kutokana na kosa la wakipingana na uongozi wa raisi wa Nchi hiyo Mh. Jose Eduardo dos Santos.
Tukio hilo la kushambuliwa kwa tovuti za Nchi ya Angola limepokelewa kwa Maskitiko makubwa sana na wana usalama mtandao wa Nchi za Afrika na imeonekana changamoto iliyojitokeza iwe ni funzo kua mataifa ya afrika bado yanahitaji jitihada za dhati kuhimili vishindo vya wahalifu mtandao.
NEWS UPDATES:
A Portuguese branch of the Anonymous hacking group says it has shut down about 20 Angolan government websites in retaliation for the jailing of 17 youth activists for plotting a rebellion against President Jose Eduardo dos Santos' government.
-------------------------
GHANA ilipata kuathirika na tukio la kuangushwa tovuti zake mwaka jana kitu ambacho kilipelekea Nchi hiyo kupitia Makamu wake wa Raisi kujipanga zaidi kuhimili vishindo vya kihalifu mtandao.
TANZANIA Imepata kuathirika na tatizo la kuingiliwa tovuti kadhaa kipindi cha nyuma na kusababisha tovuti husika kushindwa kutoa huduma na mara nyingine kuingiziwa vitu visivyo faa.
KENYA Pia Ilipata kuathirika kwa kiasi kikubwa kwa tovuti zake kitu kilicho sababisha baadhi ya tovuti kufungwa moja kwa moja – Tulipata kujadili hili kwa kina nilipo udhuria mkutano wa usalama mitandao wa Nchi za Afrika mashariki uliofanyika mwaka jana nchini Kenya.
UGANDA, kuimarisha amani ya nchi hiyo kipindi cha uchaguzi mwaka Huu ililazimika kufunga mitandao yake ya kijamii pamoja na mifumo mingine ya kimtandao ikiwa ni hofu ya amani kuyumba. Huu ni mfano ulio hai wenye mazingatio makubwa ndani yake.
AFRIKA kwa ujumla wake matukio kadhaa yamepata kutokea nabado yame endelea kutokea ambapo ni zao la kutotiliwa mkazo swala zima la ulinzi mitandao kwa Nchi zetu barani Afika kitu ambacho nadhani imefika wakati pakatiliwa manani mapendekezo ambayo yamekua yakitolewa ili kuweza kubakisha bara letu salama kimtandao.
Sign up here with your email