MAPYA YAIBUKA VIDEO QEEN WA ,HUKU KWETU, YA RAYMOND, ATOKA NA DIAMOND - Rhevan Media

MAPYA YAIBUKA VIDEO QEEN WA ,HUKU KWETU, YA RAYMOND, ATOKA NA DIAMOND


Mashabiki wa Zari the Bosslady wanamshambulia Lynn, mrembo aliyetumika kwenye video ya ‘Kwetu’ ya msanii wa WCB, Raymond kwasababu wamesikia tetesi kuwa amechepuka na Diamond Platnumz.

Tetesi hizi ni kubwa kiasi ambacho watu walio karibu na mastaa hao wamedai kuwa zimeitikisa ikulu ya Chibu. Wanadai kuwa Zari amekerwa na tetesi hizo na kwamba uhusiano wao umepata dosari.

Wiki hii tetesi hizo zimevuma zaidi kiasi ambacho mashabiki wa Zari wamekuwa wakimmiminia matusi Lynn kwenye akaunti yake ya Instagram.

Inafurahisha kwasababu Lynn haoneshi kutikiswa na matusi hayo huku pia akipewa support kubwa kutoka kwa mashabiki ambao hawampendi Zari. Of Course Team Wema yote inaonesha kuwa nyuma yake!

Cha kuvutia zaidi ni kuwa Lynn ni msichana mdogo na mrembo sana kiasi ambacho wasiompenda Zari wanasema anafaa zaidi kuwa kifaa cha Bin Mondi. Kwa wengi hizi bado ni tetesi tu lakini kama ukiangalia post za nyuma za Lynn, utagundua kuwa alikuwa shabiki mkubwa wa Daimond kwakuwa amekuwa akiweka picha zake [Diamond] mara kwa mara.



Previous
Next Post »