MAOFISA WAWILI WA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WAKAMWATA MBEYA. - Rhevan Media

MAOFISA WAWILI WA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WAKAMWATA MBEYA.

Maofisa wawili wa wakala wa huduma za Misitu nchini, TFS, pamoja na wafanyabiashara watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Mbeya, Nyerembe Mnasa Sabi, baada ya kuwakamata na shehena ya Magogo, Mbao na Mkaa ambayo inadaiwa kuandaliwa kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Nyerembe Mnasa Sabi akishirikiana na maofisa wa mamlaka ya huduma za misitu TFS kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam, wamefanya msako wa kustukiza katika maghala mbalimbali jijini Mbeya na kukamata shehena ya mazao ya misitu kama vile Magogo, Mbao na Mkaa ikiwa imehifadhiwa na nyingine ikipakiwa kwenye magari tayari kwa safari, huku wahusika wakikosa nyaraka muhimu zinazowapatia uhalali wa kumiliki rasilimali hizo, hali ambayo ikamlazimu mkuu huyo wa wilaya kutoa amri ya kuwakamata.
Maofisa wa TFS kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam wamesema kuwa wamepata taarifa za uwepo wa mazao hayo ya misitu kutoka kwa raia wema na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kila wanapoona rasilimali za Taifa zikihujumiwa.
Akijitetea mbele ya Mkuu wa wilaya, Kaimu Meneja wa TFS kanda ya nyanda za juu kusini, Deusdedit Mloge amesema kuwa kazi ya mamlaka hiyo ni kupiga mihuli kwenye mbao na magogo pamoja na kutoa kibali cha kusafirisha mazao ya misitu kwa watu wanaojihusisha na biashara hiyo.
Previous
Next Post »