MANCHESTER UNITED WAKWAMA KWENYE FOLENI. - Rhevan Media

MANCHESTER UNITED WAKWAMA KWENYE FOLENI.

Man UtdImage copyright
Image captionManchester United walichapwa 3-0
Wachezaji wa Manchester United walikwama kwenye foleni wakielekea White Hart Lane eneo la Tottenham, London kwa mechi dhidi ya Tottenham Hotspur, mechi ambayo walilazwa 3-0.
Hatua hiyo ilifanya mechi hiyo iliyopangiwa kuanza saa kumi na mbili jioni kuahirishwa hadi saa kumi na mbili na robo lakini wakawa bado hawajafika na ikaahirishwa tena hadi saa kumi na mbili unusu ambapo wakati huo waliweza kufika na mechi ikaanza.
Kiungo wa kati wa Manchester United Jesse Lingard alithibitisha kwamba basi lao lilikwama kwenye foleni kwa zaidi ya saa mbili.
“Ilikuwa jinamizi. Maandalizi yetu yamevurugika,” alisema.
Meneja Louis van Gaal akizungumza kabla ya mechi kuanza alisema ingebainika tu baada ya mechi iwapo kuchelewa kwao kuliwaathiri.
"Tutaathiriwa vipi na kuchelewa huku? Tunaweza tu kusema baadaye! Tottenham pia wamekuwa na shida kwani lazima watusubiri, nasi lazima tuharakishe.
"Tayari nimekumbana na hali sawa nikiwa na Barcelona dhidi ya Arsenal kwa hivyo nilijua jinsi London wakati mwingine huwa. Siamini! Tumezunguka jiji. Ni jambo la kushangaza kwamba huwezi ukafika unakotaka.
"Lazima tubadilishe mpango wetu wa kupasha misuli moto. Mimi si miungu, mimi ni meneja tu lakini lazima tucheze vyema kwani Tottehman ni moja ya timu nzuri zaidi kwenye ligi.”
Manchester United waliumbuliwa na mabao matatu ya haraka ya Dele Alli (70'), Toby Alderweireld (74') na Erik Lamela (76').
Van Gaal hakuzungumzia suala la foleni baada ya mechi.
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino, alipoulizwa iwapo kuchelewa kwa mechi kuliwafaa alisema: “Ilikuwa vigumu kwa sababu unalazimika kubadili baadhi ya mambo lakini kwa timu zote mbili mambo hayakuwa rahisi. Kukaa kwenye basi mkiwa mmekwama kwenye foleni. Nadhani tulicheza vyema.”
Previous
Next Post »