MAMLAKA YAINGIA MGOGORO NA WANANCHI. - Rhevan Media

MAMLAKA YAINGIA MGOGORO NA WANANCHI.



Na Woinde Shizza, Karatu

Wananchi wa kijiji cha Losteti kilichopo katika kata ya mbulumbulu wilayani karatu mkoani Arusha wamelalamika mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro kwa kitendo cha kuwanyanganya eneo lao la kuchungia mifugo lijulikanalo kwa jina la Olorieni lililopo ndani ya kijiji hicho.

Wananchi hao waliyasema hayo juzi wakati wakiongea na waandishi wa habari kijijini hapo na kusema kuwa mamlaka hiyo ya hifadhi ya ngorongoro wamewanyanganya eneo hilo ambalo walikuwa wanatumia kama eneo la malisho ya mifugo yao kwa kipindi cha muda mrefu kwani walianza kulitumia tangu enzi za mababu zao .

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Aron Saiteu Alisema kuwa eneo hilo la malisho ya mifugo ni lakwao kwa mdua mrefu lakini wanashangaa kuona hifadhi hiyo ya ngorongoro imekuja na kuwanyanganya hali ambayo inawafanya hata wao kukosa sehemu ya kufugia mifugo yao.

Walisema kuwa walishapeleka malalamiko mara kwa mara katika ofisi za viongozi wa serekali pamoja na ofisi za hifadhi hiyo lakini amna hatua yeyote ambayo imechukuliwa wala kupewa majibu ambayo yanawapa matumaini hali ambayo imepeleka wananchi hao kuumia na kukata tamaa ndani ya nchi yao.



Previous
Next Post »