MAMA ANNA KILANGO MALECELA AJITETEA BAADA YA KUTUMBULIWA. - Rhevan Media

MAMA ANNA KILANGO MALECELA AJITETEA BAADA YA KUTUMBULIWA.




Akiongea na kituo cha radio cha Times Fm,Kilango amedai kuwa hana taarifa juu ya utenguzi wa nafasi hiyo kutoka kwa aliyemteua.

“Jamani Mimi sina taarifa sipendi kukizungumzia maana yake sijaambiwa na aliyeniteua, sina la kukwambia.” Alisema na kukata simu.

Anne Kilango Malecele amedumu kwenye nafasi hiyo kwa majuma kadhaa, hata mwezi mmoja hajafikisha.


Mwanasiasa huyu Mkongwe amekumbwa na Panga hili baada ya kutoa taarifa hadharani kuwa, Mkoa wa Shinyanga haukuwa na watumishi hewa.

Kauli ambayo ilikinzana na tume rasmi ya uchunguzi iliyotumwa mkoani humo, ambapo iligundua watumishi hewa 45 na bado uchunguzi Zaidi unaendelea.
Previous
Next Post »