MAHAKAM YAMTIA HATIANA MBUNGE WA UBUNGO SAED KUBENEA. - Rhevan Media

MAHAKAM YAMTIA HATIANA MBUNGE WA UBUNGO SAED KUBENEA.



Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amehukumiwa kifungo cha nje cha miezi mitatu, akitakiwa kutokufanya kosa la kutumia lugha ya matusi baada ya kutiwa hatiani kwa kumtukana aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Adhabu hiyo ilitolewa jana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Jamhuri kumshtaki ikidai kuwa Desemba 14, mwaka jana katika kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd kilichopo Mabibo External, Kubenea alimtolea lugha chafu Makonda, ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni kibaka, mjinga, mpumbavu na kwamba nafasi yake ni ya kupewa.
Kabla ya kupewa kwa adhabu hiyo na Hakimu Mkazi, Thomas Simba, Kubenea aliiomba Mahakama impe adhabu nafuu ambayo itamfanya aendelee kuhudumia wananchi wake.
Katika hukumu yake, Hakimu Simba alikubaliana na ombi la mshtakiwa huyo na kumhukumu adhabu ya kifungo cha nje cha miezi mitatu akimtaka kutojihusisha na kosa kama hilo.
Previous
Next Post »