
Kwa mara ya kwanza aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, amezungumzia kutumbuliwa kwake kulikofanywa na Rais Dk. John Magufuli, kuwa ni kawaida kihistoria na haoni ajabu juu ya hilo.Balozi Sefue aliyasema hayo wakati akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam juzi baada ya kumalizika kwa hafla ya kuwatunuku vyeti vya shukrani wadau mbalimbali wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, akiwamo Balozi Sefue, vilivyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).“Kama unajua ilivyokwenye historia, kwa kawaida marais wakishaingia madarakani, wanakuwa na Katibu Mkuu Viongozi waliowakuta kwa kipindi cha mpito, lakini baadaye wanakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi wa kwao, kwa hiyo siyo jambo la ajabu kwangu,” alisema.Alipoulizwa juu ya maisha ya uraiani, alisema: “Hayo wakati wa kuyazungumza bado…kuhusu majukumu mengine nikipangiwa mtayasikia.” Balozi Sefue aliteuliwa kuendelea na nafasi hiyo Desemba 30, mwaka huu, baada ya kuitumikia wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Dk. Jakaya Kikwete.
Sign up here with your email