KOCHA WA KIKAPU MMAREKANI KUWASILI LEO NCHINI. - Rhevan Media

KOCHA WA KIKAPU MMAREKANI KUWASILI LEO NCHINI.



Kocha Mmarekani Mathew Mc Collister anatarajiwa kuwasili nchini hii leo kuanza kazi ya kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Mpira wa kikapu Tanzania.

Kamishna wa ufundi wa mashindano wa chama cha mpira wa kikapu nchini TBF Manase Zabron amesema, kocha huyo atawasili na kwenda moja kwa moja katika ofisi za baraza la michezo nchini BMT kwa ajili ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.
Manase amesema, wanaamini kwa uwezo wa kocha huyo ataweza kuisaidia timu hiyo kuweza kufikia malengo waliyojiwekea ya kuweza kuipeperusha vizuri bendera ya nchi katika mashindano mbalimbali.
Previous
Next Post »