
Mwenyekiti wa kijiji cha Makibo wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, Petro Ntakulo ameuawa kwa kukatwa mapanga na mwili wake kuchomwa moto na watu wasiojulikana na kisha kutoweka.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa ilisema tukio hili limetokea Machi 27 mwaka huu, saa 4:30 usiku katika kijiji cha Makibo kilichopo kata ya Nyauha wilayani Sikonge.Akielezea tukio hilo, alisema ilitokea sintofahamu iliyosababisha watu kukusanyika kujua nini kimetokea ndipo watu hao wasiojulikana walimvamia mwenyekiti huyo kisha kumkatakata mapanga na kuuteketeza mwili wake kwa moto.Kamanda Issa alifafanua kuwa hadi sasa chanzo cha mauaji hayo hakijulikani na kwamba maofisa wa Jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi wanaendelea kufanya uchunguzi.
Sign up here with your email