KAMPUNI ZA ULINZI HAZIRUHUSIWI NDANI YA OFISI ZA BANDARI. - Rhevan Media

KAMPUNI ZA ULINZI HAZIRUHUSIWI NDANI YA OFISI ZA BANDARI.



Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imesema kuwa makampuni binafsi ya ulinzi yanayofanya kazi bandarini hayahusiki na ulinzi wa sehemu nyeti za za Mamlaka hiyo.

Akitoa ufanuzi huo leo jijini Dar es salaam, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Janeth Ruzangi amekiri kuwepo kwa makamuni yanayofanya kazi ya ulinzi bandarini akifafanua kuwa hayahusiki kwa namna yoyote ile kulinda sehemu za ndani za ofisi zilizoko bandarini.

“Ninapenda kuwafahamisha wananchi kuwa Bandari inalindwa na walinzi wa aina tatu ; Jeshi la polisi, Polisi wasaidizi walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (Auxilliary Police) pamoja na walinzi wa Makampuni binafsi”

Ameongeza kuwa makampuni binafsi ya ulinzi hayalindi sehemu nyeti za bandari bali yanalinda nje ya bandari kama ilivyo kwenye ofisi zingine.

Ameongeza kuwa,polisi walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania wako kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na Bunge na wamepata baadhi ya mafunzo ya kipolisi.

Ikumbukwe kuwa agizo la kuwandoa walinzi wa makampuni binafsi kwenye maeneo nyeti ya bandari lilitolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mwezi Februari mwaka huu.


Previous
Next Post »