KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE HAIJIRIZISHWA NA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA MAOFISA ( MKATABA WA LUGUMI ENTERPRISES ) - Rhevan Media

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE HAIJIRIZISHWA NA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA MAOFISA ( MKATABA WA LUGUMI ENTERPRISES )



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) haijaridhishwa na majibu yaliyotolewa na maofisa wa juu wa Jeshi la Polisi kuhusu Mkataba wa Lugumi Enterprises, na hivyo kamati hiyo imeamua kuunda kamati ndogo leo itakayochunguza kwa undani sakata hilo.Kwa mujibu wa taarifa gazeti hili ilizopata kutoka chanzo cha kuaminika, PAC haikuridhishwa na majibu ya hoja nyingi zilizotolewa na watendaji wakuu akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhusu mkataba wa Lugumi baada ya kukutana nao jana mjini hapa.“PAC imelazimika kuunda kamati ndogo kesho (leo), itakayokuwa na nguvu kuhoji mambo yote ukiwemo mkataba huo kwa sababu majibu yaliyotolewa hayakuridhisha,” kilieleza chanzo hicho.
Kiliongeza kuwa baadhi ya mambo yanayokanganya PAC ni kufahamu nani mkweli kati ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kupitia taarifa ya ukaguzi na maelezo ya Jeshi la Polisi kuhusu gharama za mkataba.Kwa mujibu wa chanzo chetu, taarifa ya CAG inaonesha kuwa mkataba huo ni wa Sh bilioni 37.742 wakati maelezo yaliyotolewa na viongozi wa Jeshi hilo walipohojiwa na PAC hiyo jana, walisema ni Sh bilioni 37.163.Hivyo kuwepo kwa tofauti ya zaidi ya Sh milioni 578.972. Aidha, utata mwingine ni jeshi hilo kukosa maelezo ya kwa nini katika kutafuta mzabuni kwenye mradi huo, walitumia mfumo wa mzabuni mmoja badala ya wengi.
Previous
Next Post »