HII NDIYO ATHARI YA VIRUSI VYA ZIKA. - Rhevan Media

HII NDIYO ATHARI YA VIRUSI VYA ZIKA.


Image captionMbu anayesambaza ugonjwa huo huenda amesambaa katika majimbo mengi ya Marekani kinyume na ilivyotarajiwa.

Virusi vya Zika vinasababisha madhara maengi kuliko ilivyodhaniwa, wamesema maafisa wa afya Marekani.
Kwa mujibu wa Tasisi ya kuthibitri magonjwa{CDC}, Zika inasababisha dosari nyingi sana za maumbile.
Aidha mbu anayesambaza ugonjwa huo huenda amesambaa katika majimbo mengi ya Marekani kinyume na ilivyotarajiwa.
Homa ya Zika ililipuka nchini Brazil mwaka uliopita na imesababisha dosari nyingi za maumbile miongoni mwa watoto hususan kanda ya Amerika kusini.

Image copyrightAP
Image captionKufikia sasa visa 346 vya Zika vimeripotiwa nchini Marekani

Kufikia sasa visa 346 vya Zika vimeripotiwa nchini Marekani na vinahusishwa na watu kusafiri katika nchi zilizoathirika na ugonjwa huo.
Mapema mwaka huu Rais Barack Obama aliomba Baraza la Congress kupitisha bajeti ya dharura ya dola bilioni 1.9 ili kusaidia kukabiliana na virusi hivyo.
Hapo mwezi februari kulipatikana kisa cha maambukizi ya Zika ambayo yalitokana na ngono na siyo kutoka kwa mbu.
Previous
Next Post »