GARI YA MIZIGO LATEKETEA KWA MOTO KATIKATI YA MBUGA. - Rhevan Media

GARI YA MIZIGO LATEKETEA KWA MOTO KATIKATI YA MBUGA.




Gari la Mizigo lililokuwa linasafirisha shehena ya bidhaa mbalimbali kutoka Dar es Salaam kwenda nchini Zambia limeungua kwa moto baada ya kutokea hitilafu ya kiufundi katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi Mkoani Morogoro na bidhaa zote zilizokuwa ndani ya Gari hilo zimeteketea na hakuna mali iliyookolewa.
Akiongea na ITV katika mji mdogo wa Mikumi Mkoani Morogoro Dereva wa Gari hilo la mizigo Francis Semkiwa amesema gari hilo lilipata hitilafu ya ghafla usiku wa kuamkia jana baada ya kupita kwenye matuta ya barabarani katika hifadhi hiyo na ilianza kuwaka moto ambao umeteketeza mali zote ikiwemo nguo aina ya mitumba na viatu vilivyokuwa kwenye gari hilo lenye namba za usajili T 806 DEP lakini watu wote watatu waliokuwemo kwenye gari hilo wamenusurika na ajali hiyo.
 
Kwa upande wake Msemaji wa Kampuni inayomiliki gari hiyo ya jijijini Dar es Salaam Gelan Hamad amewashukuru wadau mbalimbali ikiwemo Jeshi la Polisi na hifadhi ya taifa ya Mikumi kwa ushirikiano walioutoa wakati wa tukio na kwamba mawasiliano na mteja wao mmiliki wa mali zilizoteketea aliyeko Ndola nchini Zambia yanaendelea. 
 
Kutokana na ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara katikati ya hifadhi ya Taifa ya Mikumi na kusababisha uharibifu wa mali na miundombinu ikiwemo ile ya gari lililogonga na kuua nyati wanane, baadhi ya wadau wa uhifadhi wamekuwa wakishauri serikali kuridhia mpango wa barabara hiyo kuhamishwa na kupita wilayani kilosa ili kuepuka matukio ya ajali na vifo vya watu na wanyamapori na pia uharibifu wa mali lakini pia utalii wa bure na uchafuzi wa mazingira
 


Previous
Next Post »