Mkuu wa Umoja wa Ulaya sera za kigeni , Federica Mogherini,amewasili Tehran kwa ajili ya mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya Umoja wa Ulaya na Iran yaliyodumu katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja sasa.
Mogehrini ameambatana na makamishna wa umoja wa ulaya wasiozidi saba.katika mazungumzo yao wanatarajiwa kuliangazia suala la biashara, nishati na mazingira, maeneo ambayo pande zote mbili zina nia ya kuchunguza endapo Iran imetimiza ahadi zake chini ya mkataba wa mwaka wa masuala ya nyuklia.
Pamoja na mambo mengine Mogherini , anatarajiwa kujadili namna Tehran inavyoweza kutumia ushawishi wake kuhitimisha vita vya Syria, mahali ambako maelfu ya watu wameyakimbia makaazi yao na kukimbilia Ulaya.
Sign up here with your email