DEREVA AFARIKI AKIJARIBU KUVUKA MTO KWA GARI. - Rhevan Media

DEREVA AFARIKI AKIJARIBU KUVUKA MTO KWA GARI.



Picha na Maktaba
Dereva mmoja mkoani Morogoro amefariki dunia wakati akijaribu kuvuka mto kwa gari wakati mvua kubwa ikinyesha.
Dereva huyo alikuwa akivuka mto huo ukiwa umefurika maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali.
Kikosi cha jeshi la polisi linafanya uokozi wa kuopoa mwili na gari lililozama katika mto ambapo mashuhuda wa tukio hilo wameiomba serikali kuweka kingo za vyuma pembeni mwa daraja hilo ili kuzuia ajali za kutumbukia magari.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba tukio hilo ni la kusikitisha ambapo amewatahadharisha wananchi mkoani humo kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini wakati wanapovuka mito kutokana na mito mingi kujaa maji.



Previous
Next Post »