
Kamati ya Bunge yataka TANESCO itumbuliwe kufuatia uamuzi wa kununua transfoma nje wakati zinapatikana kiwanda cha TANELEC Arusha. Wamesema “Tunashindwa kuilewa Tanesco kwanini wanafanya hivyo wakati kiwanda ni cha kwao na wakati Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Felchismi Mramba yuko ndani ya bodi ya wakurugenzi, hapa kuna mgogoro ambao unapaswa kutatuliwa kwa wakati ili kunusuru kiwanda hiki” Kamati hiyo ya Bunge imebaini hayo wakati wa ziara yao ya kutembelea viwanda jijini Arusha ili kufahamu changamoto na kasi ya ukuaji wa viwanda ambapo Wabunge hao wameshangazwa na kitendo cha Tanesco kutonunua transfoma katika kiwanda hicho ambazo huuzwa katika nchi jirani za Kenya, Zambia Malawi na Burundi.
Sign up here with your email