
Mkazi wa kijiji cha Nyabubinza wilayani Maswa mkoani Simiyu, Marco Jidendela (25) ametupwa jela maisha baada ya kupatikana na hatia ya kulawiti mtoto wa miaka 9.
Hukumu hiyo imetolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Maswa,Tumaini Marwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka.Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha mashitaka, Mkaguzi wa Polisi,Nassib Swedy kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 8 mwaka huu majira ya saa 4:30 asubuhi katika kijiji cha Nyabubinza.Mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa siku ya tukio mshitakiwa alimshika kwa nguvu mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 9 (jina linahifadhiwa) ambaye alimkuta akichunga ng’ombe na kumweleza ya kuwa achague moja amuue au amlawiti.
Kufuatia hali hiyo alitimiza adhima yake kwa kumwingilia kinyume cha maumbile na kumsababishia mtoto huyo michubuko na uvimbe katika sehemu yake ya njia ya haja kubwa kinyume na kifungu cha 154(1)(a) cha kanuni ya adhabu sura ya 16.
Nassib aliiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
Sign up here with your email