UJUMBE TOKA KWA MEYA WA KINONDONI. - Rhevan Media

UJUMBE TOKA KWA MEYA WA KINONDONI.

SAUTI YENU
NI WIKI YA BAJETI 2016/2017 YA MANISPAA YENU KINONDONI
kama mlivyo tupa ridhaa,kwamba UKAWA tutaongoza Kinondoni Municipal,tangu tuchaguliwe kuongoza halmashauri yetu hii,tunakutana na tukio kubwa la kihistoria nalo ni kupanga bajeti ya halmashauri ya manispaa ya kinondoni,wiki hii.
Bajeti yetu ya mwaka huu itakuwa TOFAUTI na watu walivyozoea kuona za miaka ya huko nyuma,ingawa taratibu za kupata bajeti zitakuwa ni PYRAMID STYLE,kwamba bajeti imeanzia ngazi ya mitaa,mikutano ya wananchi kwa mtindo wa fulsa na vikwazo (O&OD).
Baada ya hapo bajeti inakuja ngazi ya kata diwani na wenyeviti wa mitaa,na watendaji kata,mitaa na maafisa ugani, kwemye WARD DEVELOPMENT COMMETEE(WDC)
Baada ya hapo inakuja sasa ngazi ya halmashauri kupitia afisa mipango na mchumi wa halmashauri.
Mchumi wa halmashauri atachambua miradi iliyo ibuliwa kwenye kata,na kupanga kuwa miradi rasmi ya halmashauri,kwakutumia,MPANGO WA MAENDELEO YA MILLENIA 2025,(millenium devlopment goal),mpango wa mkukuta na mkurabita,matokeo makubwa sasa BRN,na kwakutumia ILANI YA UKAWA2015
Hapo ilani ya ukawa ndiyo sehemu kubwa ya mantiki ya andiko hili..
KWAMBA CCM walisha poteza uhalali wa kisiasa wa kufanya maamuzi kwenye ngazi ya WILAYA YA KINONDONI,kama mapishi yao waliyoyapika 2010-2015,wananchi wa manispaa ya kinondoni wamechoka na hawayataki tena,sasa jikoni kuna mpishi mpya naye ni UKAWA,na tunapoingiliwa mapishi yetu namtu ambaye Mwananchi hawakumpa ridhaa ya kuyapika,ndiyo maana tunakuwa wakali kwa "bwana mdogo" sababu tunajua kuingia kwake jikoni hakuwezi kuwa kwa nia njema,huenda akaweka pili pili kwenye chai kwa makusudi,au akatia sukari kwenye rosti ya nyama,ili wananchi waone hatujui kupika,na kama proposal zake zingekuwa na mantiki zingesaidia chama chake kisipoteze viti vya udiwani na ubunge.
Hivyo basi kwa mwaka huu wa fedha ILANI YA UKAWA MANISPAA YA KINONDONI,vipaumbele vitakuwa ni maeneo 10 yafuatayo,ukiondoa "outburst ya makusanyo"mapato ya ndani ambapo next week nitawapitisha kila chanzo na fedha zake.huku mikakati madhubuti ya kubana matumizi,na kuzuia ufujaji.
1.Kutengwa fedha kwa ajili ya kuiboresha miundombinu ya wamachinga na Mama ntilie
2.kutengwa fedha zairadi ya maji pembezoni mwa mji,na sehemu amabazo miradi ya maji(mabomba ya maji ya mchina hayakupita)
3.ujenzi wa Barbara za lami za mitaa kupunguza foleni(feeder roads),ukiachana na hizi za WORLD BANK,zinazo subilia tuweke FIDIA YA BILLIONI 14,kama mkopo wa manispaa kutoka benki za ndani,ili sasa tuweze kuingiziwa dollar milllioni300.
4.Mikopo ya akina Mama na vijana, kutoka asilimia tano(5%)ya makusanyo ya ndani kutokana,ambapo tayari manispaa INA amana ya BILLIONI 7.5 DCB bank,jumlisha na BILLIONI 5 tunazo enda kutenga mwaka huu,hivyo jumla ya akina Mama hamsini elfu na vijana hamsini elfu kunufaika na mikopo hii ya halmashauri,yenye riba ndogo tofauti na bank zote,na kwamba sasa mikopo inajazwa kuanzia ngazi ya kata,ili kila kata ipate million 200.
5.ununuzi wa mitambo na Magari ya taka kupunguza lundo la taka kwa siku,ambapo sasa lundo la taka ni tani 2026 kwa siku,ila manispaa hubeba tani 700 pekee kupeleka dampo,hivyo mbali na like kiwanda kuchakata taka kuwa mbolea kule Mabwepande,sasa tunaongeza ufanisi kupitia manunuzi hayo,pamoja na kuongeza bajeti ya usafishaji kumudu kulipa makandarasi wenye uwezo na kuondokana na wale uchwala.
6.kuanzisha machinjio kubwa ya kisasa yenye hadhi ya kitaifa,ndani ya halmashauri yetu,ili kuweka ubora wa huduma za nyama,na kutanua wigo wa ajira kwa vijana wetu.
7.Elimu,Elimu na Elimu
Mpango wa "Zero desk" ambapo mikakati wa kuiboresha miundombinu ya elimu ndani ya manispaa kwa kuweka fedha kunua viambajengo"facilities"kama madawati kuhakikisha hakuna hitaji tena dawati ndani ya manispaa ya kinondoni,ukarabati wa mashule ya misimgi na sekondari,kufanana na ubora wa elimu yenyewe,baada ya kuwaita wananchi wafuate elimu bure,
Kuiboresha ubora wa kumudu ushindani PRIMARY ENGLISH MEDIUM ya oysterbay,ikiwa kuongeza nyingine kama hii pembezoni mwa manispaa.
Kusimamia haki za walimu,kama rikizo na malimbikizo pamoja na upandishwaji wa madaraja kwa mujibu wa Sheria na kanuni za Utumishi.
7.Afya,kuzijengea zahanati za kata uwezo wa kufanya kazi masaa 24,badala ya utaratibu wa sasa,na kutenga fedha kwa kituo cha afya, Sinza,hospitali ya palestina kuwa na hadhi ya wilaya,ilikuweza kupokea rufaa,baadavya hii tuliyonayo mwananyamala kuipandisha hadhi kuwa hospitali ya mkoa.kununua Magari ya wagonjwa na kupangwa kwa zones,"mpango wa kila jimbo ambulance moja"Kubebea wagonjwa kutoka zahanati za kata kwenda rufani ya palestina na mwananyamala
8.Michezo,ni pamoja na kuandaa fedha kwa ajili ya kurabati wa viwanja vya michezo ngazi ya kata,kuipa motisha ya miundombinu timu ya halmashauri KMC FC(kino boyz) inayoshiriki ligi daraja la kwanza ilikuiwezesha kufudhu ligi kuu vodacom kuu,ndani ya kipindi chetu cha uongozi wa halmashauri.
9.Ardhi na mipangomiji,bajeti imetenga kupunguza migogoro ya Ardhi,na makazi holela,kwa kuwa manispaa inaeneo la asimia 17,pekee ndilo lililopimwa,hivyo kupangwa mji upya na kufungua njia kwenye makazi holela,pamoja,kuratibu programu ya urasimishaji wa makazi maeneo ambayo bado haya pimwa,kuwezesha kila Mwananchi kumiliki Ardhi kwa hati.
10.uboreshaji wa masoko 24 ya manispaa na uwekezajiwa viwanja 21vya manispaa,ambapo sasa masoko yote kuwekwa mapaa ya aina moja ya kisasa pamoja nankusakafia chini,kuondoa kero ya matope wakati wa mvua na majira mwingine,lakini uboreshaji wa mazingira ya kazi masikini,kuongezeka thamani ya bidhaa za wafanyabiashara wetu.
NB
Vipaumbele hivi ndiyo vitakavyoongoza mijada,bado kiasi na namna gani ya utekelezaji tunategemea vikao halali vitakavyoanza kukaa wiki hii,na kupitishwa rasmi,hii ni njia tuh inayotoa fulsa
KAMA kuna maeneo unaona kama UKAWA ndani ya halmashauri yetu tukifanyia kazi,itatoa unafuu mkubwa wa maisha kwa wananchi wetu wa manispaa ya kinondoni,unaweza kutushauri kuelekea wiki ya bajeti,ili kuweza kujuisha michango yenu.hivi ni vipaumbele vyetu,wewe je?
Na Boniface jacob
Mstahiki meya
Manispaa ya kinondoni
Previous
Next Post »