UGONJWA WA KIPINDUPINDU KIMEITAFUNA SERIKALI BILIONI MBILI. - Rhevan Media

UGONJWA WA KIPINDUPINDU KIMEITAFUNA SERIKALI BILIONI MBILI.




 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael  John  akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya  Takwimu za ugonjwa  wa Kipindupindu  zinaonyesha kuwa mikoa ambayo ilikwishakupata ugonjwa imeongezeka na kufikia 23 baada ya  Mkoa wa Mtwara kuripoti wagonjwa wawili kuanzia jana tarehe 13 Machi mwaka huu,   katika wilaya ya Masasi. Mikoa ya Njombe  na Ruvuma  ndio pekee hapa nchini ambayo bado haijaripoti mgonjwa wa Kipindupindu, jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto,Dk,Neema Rusibamayila.
 Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibamayila akizungumza na wandishi wa haari (hawapo picha)  juu ya Wizara inatoa wito kwa wadau wote katika ngazi zote kushirikiana kwa pamoja katika jitihada za kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu, leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Michael  John.
Wandishi wa habari wakimsikiliza  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Michael  John, jijini Dar es Salaam leo.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
INAKADIRIWA kuwa Sh.bilioni Mbili zimetumika katika harakati za kupambana na ugonjwa wa kipindupindu tangu uliporipotiwa  kwa mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam,kwa Niaba ya Naibu Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Kaimu Katibu wa Wizara hiyo, Michael John, amesema kuwa serikali imeweka nguvu zaidi katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Amesema fedha hizo zimetumika katika kuunda tume mbalimbali katika kutoa elimu juu ya ugonjwa,vifaa pamoja na vitanda katika hospitali ambazo zilipatwa na wagonjwa wa jamii hiyo.

Kaimu Katibu Mkuu amesema Mikoa ya Kanda Ziwa imekuwa na imani potofu juu ya kuchemsha maji ya kunywa kwa kudai kuwa ugonjwa huo unatokana na hali ya hewa pamoja na wavuvi wa kanda hiyo kuwa wakinywa maji yaliyochemshwa wanazma katika mitumbwi yao au wasiweze kuvua samaki hizo.

 Amesema ugonjwa wa wa kipindupindu hapa nchini umedumu kwa takribani miezi saba (7) sasa tangu uanze mwezi Agosti,   2015.   

 John amesema hadi  kufikia  Machi  13 mwaka huu  jumla ya   watu 18,399  wameugua   ugonjwa   huo, kati   yao  watu  292  wamepoteza maisha.   

Takwimu   za   ugonjwa   huu   pia   zinaonyesha   kuwa  mikoa ambayo ilikwishakupata ugonjwa imeongezeka na kufikia 23 baada ya Mkoa wa  Mtwara  kuripoti wagonjwa wawili  kuanzia jana ya machi  13  katika wilaya ya Masasi.

Mikoa ya Njombe  na Ruvuma ndio   pekee   hapa   nchini  ambayo   bado   haijaripoti   mgonjwa   wa Kipindupindu.

Takwimu   za   wiki   iliyopita   kuanzia   tarehe   7   hadi  13   Machi   2016 zinaonyesha  kuwa,   kasi ya ugonjwa  wa   kipindupindu   imeongezeka ambapo   idadi   ya  wagonjwa   walioripotiwa   wiki   hiyo   ni  758

Ikilinganishwa na 544 wa wiki iliyotangulia ya tarehe 28 Februari hadi 6 Machi ambapo  ni ongezeko la asilimia  40. Mkoa wa Iringa ambao haukuwa   umeripoti   wagonjwa  wiki   iliyotangulia,   wiki   hii   imeripoti

Ugonjwa katika Halmashauri  ile ile ya  Iringa, ambayo bado imeendelea kuripotiwa ugonjwa wa kipindupindu pia imeongezeka kutoka 10 hadi 12. Mikoa hiyo   inaongozwa na   Morogoro (196), Dodoma, (142),   Mwanza(108),   Mara(86),   Manyara(77),  Iringa(77).   Mikoa mingine   ni   pamoja   na,   Dar   es  salaam(42),     Mbeya(16),   Arusha (10),Lindi (2), Mtwara (2) na Rukwa (2).






Previous
Next Post »