
New
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Mheshimiwa Truong Tan Sang anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini tarehe 9 Machi 2016.
Madhumuni ya ziara hiyo ni kukuza uhusiano baina ya Vietnam na Tanzania mbao umedumu kwa zaidi ya miaka hamsini tangu kuanzishwa kwake pamoja Kufungua maeneo mapya ya Ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Vietnam.
Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi huyo Barani Afrika tangu aingie madarakani mwaka 2011, ambapo nchi nyingine anayotarajiwa kutembelea ni Mozambique.
Rais Truong anatarajiwa kufuatana na mke wake Bi Mai Thi Hahn, mawaziri 4 wanaoshughulika na sekta za Kilimo, Mawasiliano Uwekezaji, Afya,Viwanda na Biashara. Aidha mgeni huyo atafuatana na ujumbe wa wafanyabiashara 30 kutoka Vietnam.
Shughuli za msingi zitakazofanyika kwenye ziara
Wakati wa ziara hiyo Rais Truong Tang San atafanya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar-es-Salaam.
Aidha, Rais Truong pia atapata fursa ya kutembelea eneo la EPZ la Ubungo kuangalia viwanda mbalimbali vinavyozalisha bidhaa za kuuza nje
Baada ya kutembelea EPZA Rais Truong atahudhuria mkutano wa biashara na uwekezaji katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na taasisi za umma na sekta binafsi kutoka Tanzania na Vietnam.
Rais Truong atamaliza ratiba yake kwa kuhudhuria dhifa ya Taifa itakayoandaliwa kwa heshima yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk.John Pombe Joseph Magufuli.
Sign up here with your email
