
Wapiga kura katika majimbo matano ya Marekani leo wanapiga kura katika hatua nyengine ya mchujo kuamuwa nani wa kuchuana katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwezi wa Novemba nchini Marekani.Warepublikan na Wademokrat wote wanapiga kura huko Kansas na Louisiana wakati Warepublikan watapiga kura Kentucky na Maine na Wademokrat watashiriki kupiga kura huko Nebraska. Uchaguzi wa leo ni wa kwanza tokea kumalizika kwa chaguzi za Jumanne Kabambe ambapo majimbo 12 yalipiga kura na kuwaweka mstari wa mbele Doland Trump wa Repulikan na Hilary Clinton wa Demokrat katika kinyan'ganyiro cha kuwakilisha vyama vyao katika uchaguzi mkuu.Vigogo ndani ya chama cha Repulikan wamekuwa mbioni kumzuwiya tajiri mkubwa Trump asiteuliwe kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi huo wa rais, akitajwa kuwa ni hatari kwa Marekani.
Sign up here with your email
