Msanii Hakeem 5 ambaye alitambulika katika muziki baada ya kufanya Collabo na msani Ali Kiba kwenye wimbo wa ‘Nakshi Mrembo’ amefunguka na kusema kuwa msanii Ali Kiba si mtu mzuri na wala hana muda nae kwa sasa.
Akipiga stori kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio ambapo leo alipewa heshima ya Bongo fleva, Hakeem 5 anadai kuwa msanii huyo kwa sasa amekuwa akijisikia sana kitu ambacho yeye kimemkera na kudai kuona kwamba msanii huyo ana roho mbaya, roho ya kukunja.
” Unajua kuna wasanii wana roho mbaya sana wanadhani kwamba ridhiki wao ndiyo wanatoa kumbe Mungu ndiye mtoaji wa ridhiki, kiukweli kabisa Ali Kiba kwa sasa sitaki hata kumsikia sababu huyu jamaa nampigia simu simu zangu hata hapokei, ujumbe wangu hajibu na kuna siku nilikutana nae studio na kumwambia naomba tufanye kazi pamoja lakini yeye aliniambia unajua, Hakeem 5 kazi tutafanya ila subiri kwanza na mambo kama hayo ndiyo maana saizi sitaka hata kumsikia” alisema Hakeem 5.
Katika hatua nyingine msanii huyo amezidi kusikistiza kuwa anataka kufanya kazi na msanii huyo na kusema kuwa yeye hataki pesa za Ali Kiba ila anachotaka kwa sasa ni kufanya nae kazi tu, kwani yeye Hakeem 5 anasema ameshamalizana na Ali Kiba kwenye wimbo wa Nakshi Mrembo ila Ali Kiba yeye bado hajamalizana na msanii huyo.
Unajua mimi nimefanya mambo makubwa na Ali Kiba na wala hakunilipa na mimi sitaki pesa zake nilimwambia sitaki pesa yako mimi nataka tufanye kazi, yeye anasema kila jambo linawakati wake, mimi nilishamalizana na yeye ila yeye hajamalizana na mimi” alidai Hakeem 5.
Sign up here with your email