SHIRIKA LA TANESCO KUJISHUSHA BEI. - Rhevan Media

SHIRIKA LA TANESCO KUJISHUSHA BEI.



Shirika la Umeme (Tanesco) limewasilisha katika Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) maombi ya kushusha bei ya umeme kwa asilimia 1.1 pamoja na kuondoa kabisa gharama za maombi ya awali ya wateja wapya na gharama za huduma kwa wateja wa majumbani.Gharama za maombi hayo ya awali ambayo pia yanajulikana kama gharama za fomu ni Sh 5,900 na gharama za huduma (service charges) ni Sh 5,520 kwa mwezi kwa wateja wa majumbani.Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanseco, Felichesmi Mramba alisema kuwa kisheria maombi hayo yanatakiwa kujibiwa ndani ya siku 24 ambapo wanaamini kuwa watapata majibu mazuri.Mramba alisema gharama za huduma zimekuwa zikiathiri sana watumiaji wa umeme wa majumbani tofauti na wanaotumia viwandani.
Mramba alisema kuwa maombi hayo yamewasilishwa baada ya Tanesco kufanya tathimini ya kina kimahesabu pamoja na kubuni namna ambayo wateja wao wataweza kupata ahueni ya gharama kwa kuzingatia mazingira ya sasa.
Previous
Next Post »