RAIS MAGUFULI SIKILIZA KILIO CHA JIPU LA MH ZITTO KABWE. - Rhevan Media

RAIS MAGUFULI SIKILIZA KILIO CHA JIPU LA MH ZITTO KABWE.



Standard Bank wachunguzwe Kwa rushwa Hati Fungani ya USD 600m Kwa Tanzania
Deni la Taifa la Tanzania sasa ni USD 15 bilioni ( tshs 30 trilioni). Kutokana na ukubwa wa deni hilo, Tanzania hulipa Huduma ya Deni la Taifa takribani tshs 2.2 trilioni kila mwaka. Bajeti ya kuhudumia Deni la Taifa ni kubwa zaidi kuliko bajeti ya Wizara yeyote nchini Tanzania.
Hata hivyo katika Madeni hayo kuna ambayo yamepatikana Kwa rushwa na mengine yamechukuliwa Kwa matumizi ya anasa tu. Kitaalam Madeni haya yanaitwa ' odious debts '. Moja ya Deni la hovyo ni USD 600m ambalo Tanzania ilikopa kutoka Benki ya Standard ya Uingereza kupitia Hati Fungani. Taasisi ya SFO ya Uingereza inayoshughulika na rushwa kubwa imeonyesha kuwa mkopo huu ulipatikana Kwa rushwa. Taasisi ya Corruption Watch ya UK imeonyesha kuwa Tanzania imepata hasara ya takribani USD 80 milioni ( tshs 160 bilioni ) Kwa kuchukua mkopo huu. Hata hivyo uchunguzi wa SFO haukuhusisha maofisa wa juu wa Standard Bank makao makuu na hivyo kufunika kombe mwanaharamu apite. Iwapo uchunguzi ungegundua kuwa Standard Bank walihusika moja Kwa moja na Hongo hii, Tanzania ingefutiwa deni lote na kuokoa fedha nyingi sana ambazo zingewekezwa kwenye sekta za elimu, afya na Maji.
Tunataka Benki ya Standard ya Uingereza ichunguzwe upya na SFO kuhusu tuhuma za rushwa ili kupata biashara Tanzania ( Hati Fungani USD 600m ).
Unataka kujua ukweli wote kuhusu ufisadi wa Hati Fungani ulioliingizia Taifa deni la USD 600 milioni ( tshs 1.2 trilioni )?
Saini petition hii ili taasisi ya Rushwa kubwa ( FSO ) ya Uingereza ifungue upya uchunguzi kwa kuzingatia ushahidi mpya kuwa mabosi wa Benki ya Standard ya Uingereza walihusika na mipango ya kutoa hongo ili kupata biashara Tanzania. Ikigundulika kuwa mabosi hawa walishiriki maana yake Tanzania itafutiwa deni lote kwa sababu benki hiyo itawajibika kurudisha fedha za watu kwani Hati fungani itaonekana ni batili. Tanzania inaanza kulipa deni hilo kuanzia mwezi Aprili, 2016 kama tusipohakikisha tunazuia Kwa kupitia petition hii. Iwapo deni hili litalipwa juhudi za Rais John Magufuli kupata mapato zitaathiriwa na sekta nyeti kama elimu, afya na Maji zitakosa bajeti ya kutosha.
Mkopo uliopatikana Kwa rushwa sio halali.
Ewe Mtanzania ungana na Watanzania wenzako duniani kutaka SFO ifungue uchunguzi kwa kuzingatia ushahidi mpya dhidi ya Benki ya Standard ambayo sasa inaitwa ICBC plc
Petition hii imeletwa kwenu na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi ughaibuni

Previous
Next Post »