NAHODHA ZA SIMBA FC ASIMAMISWA KAZI. - Rhevan Media

NAHODHA ZA SIMBA FC ASIMAMISWA KAZI.



Katika taarifa yake Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Klabu Simba Haji Manara amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya mchezaji huyo kumtolea maneno yasiyo na staha kocha wa Simba Jackson Mayanja kabla ya mechi ya Jana ya kombe la shirikisho dhidi ya Singida United.
Manara amesema kutokana na kitendo hicho kisicho cha kiungwana kilichofanywa mbele ya wachezaji wenzake na kinachokiuka waraka wa maadili (Code of Conduct) kamati ya utendaji licha ya kumsimamisha mchezaji huyo pia imeagiza alipewa nusu mshahara katika kipindi chote cha adhabu yake.
Manara amesema pia kamati hiyo imewataka wachezaji wote kuzingatia nidhamu na weledi katika kipindi chote wanapoitumikia klabu ya Simba.
Previous
Next Post »