Waziri wa Elimu, Mafunzo ya Ufundi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amezuia ‘ulaji’ wa Sh4 bilioni zilizokuwa zitumike kwa ajili ya semina ya siku nne.
Akizungumza wakati akifunga mkutano mkuu wa tatu wa maofisa elimu mkoa na wilaya nchini, Profesa Ndalichako alisema amezuia mafunzo yaliyokuwa yagharimu Sh4 bilioni ambayo mtu mmoja alitengewa Sh4 milioni kwa ajili ya semina ya siku nne.
“Ina maana kila mtu alikuwa alipwe shilingi milioni moja kwa siku. Kweli hatuoni aibu kutumia fedha hizo kwa mafunzo. Watu walewale wanaokwenda kwa mafunzo yaleyale,” alisema. Alisema wakati hayo yote yakitendeka, wanafunzi wananyeshewa mvua kwa kukosa madarasa na wanakaa chini kwa kukosa madawati.

Profesa Ndalichako, pia alisema amegundua ufisadi katika Sh66 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya mafunzo, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule nchini
Sign up here with your email