Vigogo watatu akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco), Benhardard Tito, wamefikishwa kortini wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwamo kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 527,540 (sawa na Sh. bilioni 1.16).
Washtakiwa wengine ni mfanyabiashara Kanji Mwinyijuma na Katibu wa Rahco, Emmanuel Massawe.
Walisomewa mashitaka yao jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis, akisaidiana na Waendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Janeth Machurya, Maghela Ndimbo na Stanley Luoga.
Vitalis alidai kuwa kati ya Septemba Mosi, 2014 na 30, 2015, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama ya kutenda makosa kinyume cha Sheria ya Takukuru ya mwaka 2007
Sign up here with your email