KOCHA WA YANGA AIOGOPA AZAM FC. - Rhevan Media

KOCHA WA YANGA AIOGOPA AZAM FC.





Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema pamoja na ugumu unaotarajiwa kuwepo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC kesho, wamejipanga kuibuka na ushindi ili wiki ijayo wageukie michuano ya kimataifa wakiwa na ari.Yanga itacheza na APR ya Rwanda wiki ijayo na kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania kinatarajiwa kuondoka nchini Jumatano ijayo kwenda Kigali, Rwanda kuwakabili maafande hao wa jeshi la Rwanda katika mchezo wa kwanza wa mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Alisema jana kwa njia ya mtandao kuwa, ushindi katika mchezo wa kesho utakuwa na maana kubwa kwao Yanga hasa kwa kuwa mikakati yao ni kufanya vizuri katika michuano yote wanayoshiriki hivi sasa.
Previous
Next Post »