
Taarifa inatolewa kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA itakutana katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Siku ya Jumanne, Machi 1, 2016 jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa Taifa Mhe. Freeman Mbowe(MB), ambapo pamoja na masuala mengine, itajadili agenda zifuatazo;
1. Hali ya kisiasa nchini.2. Kupokea taarifa ya vikao vya mabaraza ya mashauriano ya mikoa.
3. Kupokea na kujadili Mpango Mkakati wa Chama.
4. Kupokea na kujadili taarifa ya mapato na matumizi ya chama katika kampeni za uchaguzi mkuu 2015
Imetolewa Jumatatu, Februari 29, 2016 na
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Sign up here with your email
